Monday, October 31, 2016

APPEALS DHIDI YA MAOMBI YA MKOPO IMEFUNGULIWA

The Higher Education Students’ Loans Board (HESLB) is hereby informing all loan applicants that the appeals window will be open for 90-days starting from 31st October, 2016. All Appellants should follow the below procedure: -
(i) All appeals will attract a non-refundable fee of Tzs. 10,000/= per appeal which should be paid through M-Pesa and the Transaction ID generated should be input into the Online Loan Application and Management System prior to appealing online.
(ii) You must complete the relevant Online Appeal Forms, make a printout of the same and attach thereto the necessary supporting documents.  The Online Appeals Form is accessible through http://olas.heslb.go.tz 

(iii) After successful completion of the Online Appeal Form, the appellant must download the form and attach the necessary documents and hand over to the respective Higher Education Institution Loan Desk Officer.
(iv) Appeals must be routed through the respective Loan Desk Officers who will collect all appeal forms from their respective Institutions and submit them under covering letters to the Board.  The Board will not accept any appeal forms that will be submitted directly by students to the Board. 
(v) The deadline for online submission of appeals will be 31st January, 2017.
ISSUED BY:
THE EXECUTIVE DIRECTOR
HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD
31st October 2016

Sunday, October 30, 2016

MISS TANZANIA 2016


Miss Tanzania 2016 DIANA EDWARD akiwa na wenzake waliofika Tatu Bora Grace Malikita na Maria Peter

Saturday, October 29, 2016

RONALDO APIGA HAT-TRICK YA 43


CR7 amepiga hat-trick yake ya 43 zikiwemo 31 za LA LIGA TU katika mechi ya PRIMERA DIVISION leo dhidi ya DEPORTIVO ALAVES

UJAZAJI WA DODOSO ZA MKOPO KWA WANAOENDELEA NA MASOMO

BODI YA MIKOPO - UJAZAJI WA DODOSO NDANI YA SIKU 30 - WANUFAIKA WA MIKOPO ELIMU YA JUU (KWA WANAFUNZI WANAOENDELEA)

KWA WANAFUNZI WOTE WALIOPO VYUONI
Wanafunzi wanufaika wa mkopo elimu ya juu..."hasa wale wanaoendelea na masomo",kuanzia jumatatu ijayo,tarehe 31/10/2016 kila mnufaika anapaswa kuingia kwenye akaunti yake binafsi ya HESLB ili ajaze DODOSO lililoboreshwa zaidi kwa lengo la kuwa na taarifa sahihi zaidi zinazoweza kuwa VERIFIED na vyombo vya serikali kuhusu hali ya kifedha ya mnufaika.

Baada ya dodoso hilo kujazwa, litahakikiwa na ikibainika taarifa ulizotoa ni za uongo basi mnufaika ATAPOTEZA SIFA ya kupata mkopo wake. 
Pia, kwa yoyote ambaye hatajaza DODOSO hilo pia naye ATAPOTEZA sifa ya kuwa mnufaika. Kwa hiyo ni zoezi la VERIFICATION ya taarifa za kifedha za mnufaika. Muda ukifika Dodoso hilo  litajieleza.
Hivyo,  from next Monday every beneficiary has to log into his/her account. Ni zoezi la muda wa mwezi mmoja tu na litaisha  mwezi Novemba hivyo kila mtu afanye hima kujaza dodoso hilo jipya.

Pia unatakiwa kuendelea kuhakiki majina yenu  (Kuna ya mwaka wa kwanza na wanaoendele). ili kujua kama upo chuo kihalali (kwa sifa na vigezo) au la. Zoezi hilo limeanza tayari. - hii ni kwa wanafunzi wote

WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU DODOMA


KUANGALIA TAARIFA YA MKOPO WALIOOMBA HESLB



SERIKALI YARUDISHA HISA ZAKE UDA


Serikali imefanikiwa kurejesha udhibiti wake kwenye Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) baada ya kurejeshewa asilimia 52 ya hisa zilizonunuliwa kinyume na utaratibu na Kampuni ya Simon Group Limited (SGL). 
 
Kurejeshwa kwa hisa hizo kunatokana na ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwamba mauzo ya hisa hizo yaliyofanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa Uda hayakuwa na kibali cha Serikali. 
 
Ripoti ya CAG ya mwaka 2014/15 ilibainisha licha ya utaratibu kukiukwa pia hakuna vilelezo vya fedha za manunuzi zaidi ya kuonyesha Sh320 milioni ziliingizwa kwenye akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Bodi, Idd Simba ambazo hata hivyo alidai ni malipo ya ushauri alioutoa kwa mwekezaji huo. 
 
Kurejeshwa kwa hisa hizo, kutolewa taarifa ndani ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ambayo Jumanne ya wiki hii iliuweka kikaangoni uongozi wa Jiji la Dar es Salaam kuhusiana na sakata la Uda. 
 
Pia, kamati iliwataka Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) George Simbachawene, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru wafike kwenye kamati wakiwa na majibu sahihi kuhusu sakata hilo.
 
 Viongozi hao waliitikia wito huo jana, na baada ya kikao cha faragha Mwenyekiti wa LAAC , Vedasto Mwiru alisema Serikali imeitaarifu kamati yake kuwa imerejesha katika himaya yake fungu kuu la hisa ambazo hazikugawiwa. 
 
Mwiru alisema Serikali imerejesha hisa asilimia 52 ambazo ziliuzwa na Bodi ya Wakurugenzi Wa Uda kinyume cha utaratibu. 
 
“Maelezo yaliyotolewa na Serikali zile share (hisa) zote  ambazo hazikugawiwa ziko salama chini ya mikono  salama ya Serikali hazijauzwa,” alisema. 
 
Mwiru ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CUF), alisema kutokana na maelezo hayo wabunge wametaka mikataba ya kurudisha hisa hizo kwa Serikali ipelekwe kwenye kamati hiyo. 
 
Alisema kamati hiyo inaipa Serikali muda wa wiki mbili kuhakikisha kuwa wanawasilisha nyaraka hizo. 
 
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema wanasubiri majibu ya barua yao ya kuomba ushauri kuhusu uuzwaji wa hisa za jiji za asilimia 51 kutoka kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Alisema baada ya kupokea ushauri huo watapeleka katika Baraza la Madiwani ili kuona namna ya kwenda mbele pamoja na kuzifanyia kazi fedha walizouza hisa zao ambazo ziko katika Benki Kuu (BoT). 
 
Mwanasheria Mkuu Masaju alisema anakwenda kuandika mambo yote yaliyosemwa ili iwasaidie kamati na Jiji la Dar es Salaam kukamilisha utaratibu huo kisheria.

Wednesday, October 26, 2016

UTOAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI MWAKA 2016/2017

Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa  utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:
 I. Vipaumbele vya  kitaifa vinavyoendana na Mpango  wa Maendeleo  wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya  Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji  ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa  Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
i. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji  maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo                                                 873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa  viungo                                             118
o Wadahiliwa  wahitaji wenye  mzazi mmoja                                      3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali                     87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma  kozi  za kipaumbele                      6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine                                  9,867
Jumla                                                                                             20,183
Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Saturday, October 22, 2016

Walioshinda tuzo za MTV Mama 2016

 List yote ya walioshinda tuzo za MTV Mama 2016

  1.  Winner Best Group - Sauti Sol wa Kenya  

     2.  Winner Best Pop/Alternative Act - kyle deutsch & shekhinah wa South Africa

     3.  Winner BEST FEMALE - Yemi Alade << Nominees Josey (Ivory Coast) MzVee (GH) Tiwa  (NG) Vanessa (Tanzania)

     4.  Winner BEST International Act - Drake, nominees walikua
Beyonce, Adele, Future and Rihanna.

     5. Winner Best Live Act - Cassper Nyovest 

     6. Legend Award - Hugh Masekela, a South African trumpeter, flugelhornist, cornetist, composer, and singer 

     7. Winner Best Lusophone - C4 Pedro Angola, Nominees NGA, Nelson Freitas, Lizha James and Petro Show.

     8. Winner Best Francophone-Serge (Ivory Coast), Nominees Franko (CMN) J-Rio (GBN) Magasco (CMN) and Toofan

     9. BEST MALE - WIZKID (NG), Nominees AKA (South Africa)
Patoranking (NG) Black Coffee (S.A)
Diamond (TZ)

    10. LISTENER’S CHOICE - Winner Jah Prayzah (Zimbabwe), Tuzo hii ilikua ikiwaniwa na Watanzania Yamoto Band

    11. BEST COLLABO-Dj Maphorsia ft. Wizkid Dj Buckz –Soweto Baby << Afrika mashariki iliwania hii kupitia Sauti Sol ft. Alikiba

    12. VIDEO OF THE YEAR - Winner Nique Ma Vie - Youssoupha (Congo) – Director: Antony Abdelli & Jose Eon

    13. Personality of the year-Caster Semenya << nominees Linda Ikeji, Wizkid, Pearl Thusi, Pierre Aubameyang

    14. Winner Best Group - Sauti Sol Kenya, Tuzo iliwaniwa na R2Bees (Ghana) Toofan (Togo) Navy Kenzo (Tanzania) Mi Casa (S.)

    15. BEST HIPHOP - Emtee (S.A) << ,Nominees Olamide (NG) Kiff No Beat (I.Coast) Ycee (NG)
Ricky Rick (S.A)

    16. BEST NEW ACT - Winner TEKNO (Nigeria) Tuzo hii pia ilikua ikiwaniwa na Rayvanny wa Tanzania ( WCB)

   17. SONG OF THE YEAR - MY WOMAN Patoranking, iliwaniwa pia na 'Unconditionally bae' ya Sauti Sol & Alikiba

  18. ARTIST OF THE YEAR-Wizkid, Nominees Black Coffee (S.A) Diamond (TZ) Sauti Sol (K.E)
Yemi Alade (NG) 

 

Rais Magufuli aiagiza HESLB

Rais Magufuli aiagiza HESLB kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli ameagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutumia Sheria zilizopo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni kwa wahitimu walionufaika na mikopo.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)  kwa gharama ya shilingi bilioni 10.

Amesema kuwa Serikali inadai takribani shilingi trilioni 2.6 kwa wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu.

“Serikali inawadai wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu takribani shilingi trillion 2.6 ambazo wanatakiwa kuzirudisha ili ziweze kutolewa kama mikopo kwa wanafunzi wapya na waliopo vyuoni”alifafanua Dkt Magufuli.

Aidha Dkt. Magufuli ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kusimamia ipasavyo suala la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi kwa kuzingatia vigezo vilivyopo kwani lengo la mikopo hiyo inawalenga watoto maskini.

Alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko ya kuwa  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inafanya zoezi la ugawaji wa mikopo hiyo kwa upendeleo hivyo kuzitaka uongozi wa Wizara kushughulikia suala hilo.

Mbali na hayo Rais Magufuli amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutimia mikopo hilo kwa malengo mazuri katika kujinufaisha na masuala ya Elimu.

Naye Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako  alisema kuwa mradi wa ujenzi wa hosteli hizo utasaidia kuwahudumia wanafunzi 3,840 ambapo unatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi Desemba 2016.

Katika hatua hiyo Prof. Ndalichako alisema kuwa wanafunzi waliodahuiliwa kwa mwaka huu wapo 58,000 hivyo suala la wanafunzi 66,000 kukosa mikopo hiyo ni upotoshaji unaofanya na baadhi wa watu.

Mradi wa Ujenzi wa Hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wenye majengo 20 kila jengo gorofa nne zenye vyumba 12 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Desemba mwaka huu.

Friday, October 21, 2016

BODI YA MIKOPO(HESLB) YAREJESHA POSHO VYUO VIKUU

PROFESA NDALICHAKO AONGELEA MAREJESHO YA POSHO TSH 8500

Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetuliza hasira za wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kurejesha posho ya chakula na malazi ya Sh8,500 kwa kila mmoja na kwamba tofauti baina yao itakuwa viwango vya ada.

Ufafanuzi huu uliotolewa jana usiku na Waziri wa Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza katika mahojiano maalimu na kituo cha runinga cha Taifa -TBC utakuwa faraja kwa wanafunzi ambao chini ya Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) walipanga kushinikiza walipwe posho ya Sh8,500 kwa siku kama ilivyokuwa awali. 
Hatua ya wanafunzi kujenga umoja ili kushinikiza haki katika posho ilitokana na baadhi yao kuingiziwa kati ya Sh40,000 na 70,000 badala ya Sh 510,000, hali ambayo ilizua sintofahamu. 

Ndalichako alisema tofauti ya malipo itakuwa katika ada na siyo posho,“Vigezo vya mikopo vimebadilika, kila mwanafunzi atapata fedha tofauti lakini tumefanya marekebisho kwenye posho ya chakula ambayo kila mwanafunzi atalipwa Sh8,500 kama awali.” 

Kwa mujibu wa utaratibu wa Bodi hiyo, malipo hayo ya chakula na malazi hutolewa kila baada ya miezi miwili. 

Mapema jana, Daruso iliwataka wanafunzi wa chuo hicho kutotia saini fomu za fedha za mikopo yao mpaka itakapowapa ruhusa ya kufanya hivyo. 

Rais wa Daruso, Erasmi Leon alisema hayo jana wakati akizungumza na wanafunzi wenzake kuhusu kusudio la kwenda HESLB kwa ajili ya kutafuta haki yao ya msingi. 

“Ninachowasihi tuwe pamoja. Tuwe wamoja na twende pamoja. Tutakwenda wawakilishi kutafuta nafasi kwa amani waweze kusikia tuna hoja gani lakini tukinyimwa hii nafasi tutaenda kuitafuta tukiwa wengi,”alisema na kuongeza:

 “Tuwe watulivu kwa sasa tutakapowahitaji muda na wakati wowote kwa lolote tushirikiane ili twende pamoja tumalize pamoja tuhakikishe tunapata Sh8,500 kwa kila mwanafunzi kwa chakula na malazi,”alisema. 

Kuhusu suala hilo, uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ulisema wajibu wake ni kupokea na kusambaza majina na taarifa kutoka Bodi kwa wanafunzi. 

Akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi waliofika ofisini kwake kujua hatima yao na waliopata mikopo kuchukua fomu za kutia saini, Ofisa Mikopo wa UDSM, Lugano Mwakyusa alisema wenye jukumu la kujua walio na sifa ya kupata mikopo ni Bodi ya Mikopo. 

“Tunaendelea kupokea majina kutoka bodi. Tayari hapa kuna majina 949 yameshatoka, wengine tuzidi kusubiri na wale mwaka wa pili na tatu ambao walikuwa na mitihani ya marudio taarifa zao zitapelekwa bodi,”Mwakyusa aliwaambia wanafunzi waliokuwa wamejaa ofisini kwake.

 Kulikuwa na hali ya sintofahamu chuoni hapo jana baada ya wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza kuonekana wakiwa wameshika bahasha za kaki zilizokuwa na fomu za usajili wanazotakiwa kujaza huku wakihangaika kutokana na kutojua kiasi cha mkopo. 

Juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, AbdulRazaq Badru alieleza kwamba ingawa wanafunzi 88,000 waliomba mikopo kutoka HESLB, uwezo wa bodi hiyo ni kutoa kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa na asilimia 24 na waliokuwa wameshapatiwa walikuwa 11,000 sawa na asilimia 12. 

Takwimu hizi zinaonyesha zaidi ya robo tatu ya wanafunzi wanaohitaji mikopo watakosa kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.

RAIS MAGUFULI AKIONGEA KUHUSU MIKOPO VYUO VIKUU



ALICHOZUNGUMZA RAIS MAGUFULI KUHUSU MKOPO VYUO VIKUU

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 483 kwa mwaka huu kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu ambapo wanafunzi zaidi ya 118,000 watanufaika.

Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi la hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo, Rais Magufuli amesema miongoni mwa hao watakaonufaika, wanafunzi 93,000 ni wanaoendelea na masomo na wanafunzi takribani 25,000 ni watakaoanza masomo mwaka huu huku akiweka bayana kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia masikini.

Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kurekebisha dosari zilizopo katika mfumo wa utoaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na upangaji mbaya wa wanafunzi katika vyuo, kutoa mikopo kwa upendeleo, kutozingatia sifa za mkopaji, kutoa mikopo hewa na kufungua vyuo kabla ya mikopo ya wanafunzi kutolewa na pia amewaonya wanafunzi kujiepusha na vitendo visivyofaa wakati Serikali inarekebisha dosari hizo.

"Na ndio maana wakati mwingine na wabaya wanapitia humo humo, mara fanye hivi fanyeni vile, wakati wanajua kuwa mkifanya yasiyofaa Serikali itawafukuza tu ili mkafanyie mambo yenu huko.

"Kwa sababu huwezi kuwa unahangaika kutafuta fedha za kuwapa mikopo, wakati huo huo unahitaji kujenga reli, wakati huo huo unahitaji kujenga barabara, wakati huo huo unahitaji kulipa mishahara, wakati huo huo unahitaji kutoa elimu bure, wakati huo huo Karagwe kuna njaa, wakati huo huo watu wanahitaji dawa hospitali, halafu watu wengine wanataka kukuendesha kana kwamba hela unayokusanya ni kwa ajili yao tu, ni lazima tuelewane na mimi ninataka kuwaeleza kwa dhati lazima twende katika njia iliyonyooka, ni bora uwe Rais usiye maarufu lakini utimize uliyoyaahidi, asitokee mtu wa kukuendesha, ninajua mmenielewa"amesisitiza Dkt. Magufuli.

Dkt. Magufuli ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kujipanga vizuri kukusanya marejesho ya mikopo kwa wote waliokopeshwa na bodi hiyo ambapo mpaka sasa bodi inadai takribani Shilingi Trilioni 2.6.

Wednesday, October 19, 2016

MIKOPO KUTOLEWA KULINGANA NA VIGEZO VYA WANAFUNZI

Wizara ya elimu imefafanua kuwa wametoa mikopo kulingana na vigezo vya wanafunzi na pia sio wote wenye vigezo watapata kwa kuwa bajeti ina ukomo.

Naibu waziri amesema wanafunzi wengi walikuwa wanapata mikopo pasipo na vigezo na walikuwa wakitumia mikopo kufanyia mambo mengine kama kunywa pombe kununulia tv na kutembea ambavyo sio kusudio la mikopo hiyo.




UHAKIKI WA VYUO NA WANAFUNZI WAKE WA SHAHADA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia Viongozi wa vyuo vyote vinavyotoa shahada nchini vya umma na vya binafsi kuwa kutakuwa na uhakiki wa ubora wa vyuo hivyo.   

Uhakiki huo utaanza siku ya Jumatano Oktoba 19, 2016, hivyo, vyuo vyote vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu zitakazofika kwa ajili ya kufanya uhakiki huo.

Aidha, katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuo vyote, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), itatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU katika Programu zao za Shahada katika vyuo mbalimbali vinavyotoa shahada nchini siku ya Jumanne Oktoba 18, 2016.

Hivyo, wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya TCU na kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na Uongozi wa TCU haraka iwezekanavyo ili kupata maelezo Zaidi. Mwanafunzi ambaye hatazingatia haya ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Tuesday, October 18, 2016

MAJINA YA MIKOPO VYUO VIKUU 2016/2017

MAJINA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WALIOPATA MKOPO 2016/2017

MUONGOZO WA UTOAJI MIKOPO

JUMUIA YA WANAFUNZI WA TAASISI ZA ELIMU YA JUU TANZANIA (TAHLISO)
                                                      IMG-20160330-WA0041
                    TAARIFA KWA WANAFUNZI WA TAASISI ZA ELIMU YA JUU

YAH: MUONGOZO WA UTOAJI MIKOPO ULIOTOLEWA NA WIZARA YA ELIMU ,   
                                        SAYANSI NA TEKINOLOJIA.
Jumuia ya Wanafunzi wa  Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) inawataarifu wanafunzi wote wa vyuo vikuu namna ilivyoshughulikia na kupata utatuzi wa Muongozo uliotolewa na Wizara kama ifuatavyo.
Waraka uliotolewa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Tarehe 14/10/2016 ulitoa ufafanuzi namna mkopo utakavyotolewa kwa mwaka huu 2016/2017 kwa wanafunzi wapya wanaojiunga na masomo kwa mwaka huu “kuanzia mwaka huu wa masomo ,wanufaikawote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo)watakopeshwa kulingana na uwezo wao (means tested) katika vipengele vyote vya mkopo” Kufuatia maelezo hayo ni dhahiri mikopo kwa wanafunzi wanaoendele hasa kwa wale wenye wazazi  bila kujali anauwezo ama hana uwezo mikopo yao ingepungua kutoka kwenye asilimia walizopangiwa awali, hata hivyo kwa muongozo huo ungepelekea fedha inayotolewa kwa ajili ya chakula na malazi (boom) kupungua jambo ambalo lingepelekea wanafunzi wengi kushindwa kuendelea na masomo kutokana na uwezo wa familia wanazotoka hasa watoto wa maskini ambao hutegemea fedha hizohizo za boom kulipia sehemu ya ada iliyobakia na huku wakiendelea kuishi maisha ya shida vyuoni.
TAHLISO ambayo ndio chombo cha kutetea maslahi ya wanafunzi wote wa vyuo vikuu  tumeliingilia kati swala hilo kwa kufanya mazungumzo na uongozi wa bodi ya mikopo  HESLB  pamoja na mh.Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Ndalichako juu ya kubadili msimamo wa muongozo huo kwakua utawaathiri wanafunzi wengi ambao ni watoto wa maskini.
Katika majadiliano yetu yaliongozwa na hoja mbili zinazohusu wadahiliwa wapya na wanaoendelea na masomo, tumekubalina yafuatayo:
1.      Muongozo mpya wa utoaji mikopo uliotolewa kwa mwaka huu wa masomo 206/2017 utawahusu wadahiliwa wapya wanaoanza masomo.
2.      Wanafunzi wanaonufaika na mikopo wanaoendelea na masomo wao wataendelea na utaratibu kama ulivyokuwa tangu awali walivyoingia makubaliano na utaratibu mpya hautawaathiri.
Hata hivyo zoezi la serikali la kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi mnufaika anayestahili kupata mkopo anapata mkopo wake.
Aidha kufuatia Tangazo la Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia lililotolewa tarehe 17/10/2016 linalohusu uhakiki wa wanafunzi wanaoendela na masomo ya shahada  zoezi litakalofanyika kwa wiki mbili kuanzia tarehe 19/10/2016. TAHLISO inaomba kila mwanafunzi anayesoma shahada kuangalia majina yaliyotolewa kwenye tovuti ya TCU ili kuhakikisha jina lake lipo,na kwa yule ambaye hataona jina lake awasiliane na uongozi wa TCU haraka iwezekanavyo ndani ya wiki hizo mbili kuanzia tarehe tajwa hapo juu  ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza.



STANSLAUS PETER KADUGALIZE

MWENYEKITI WA TAHLISO