Tuesday, October 18, 2016
MUONGOZO WA UTOAJI MIKOPO
JUMUIA YA WANAFUNZI WA TAASISI ZA ELIMU YA JUU
TANZANIA (TAHLISO)

TAARIFA KWA WANAFUNZI WA
TAASISI ZA ELIMU YA JUU
YAH:
MUONGOZO WA UTOAJI MIKOPO ULIOTOLEWA NA WIZARA YA ELIMU ,
SAYANSI
NA TEKINOLOJIA.
Jumuia ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) inawataarifu wanafunzi wote
wa vyuo vikuu namna ilivyoshughulikia na kupata utatuzi wa Muongozo uliotolewa
na Wizara kama ifuatavyo.
Waraka
uliotolewa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Tarehe 14/10/2016 ulitoa
ufafanuzi namna mkopo utakavyotolewa kwa mwaka huu 2016/2017 kwa wanafunzi
wapya wanaojiunga na masomo kwa mwaka huu “kuanzia mwaka huu wa masomo ,wanufaikawote
wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo)watakopeshwa kulingana na uwezo wao
(means tested) katika vipengele vyote vya mkopo” Kufuatia maelezo hayo
ni dhahiri mikopo kwa wanafunzi wanaoendele hasa kwa wale wenye wazazi bila kujali anauwezo ama hana uwezo mikopo
yao ingepungua kutoka kwenye asilimia walizopangiwa awali, hata hivyo kwa muongozo
huo ungepelekea fedha inayotolewa kwa ajili ya chakula na malazi (boom)
kupungua jambo ambalo lingepelekea wanafunzi wengi kushindwa kuendelea na
masomo kutokana na uwezo wa familia wanazotoka hasa watoto wa maskini ambao
hutegemea fedha hizohizo za boom kulipia sehemu ya ada iliyobakia na huku
wakiendelea kuishi maisha ya shida vyuoni.
TAHLISO
ambayo ndio chombo cha kutetea maslahi ya wanafunzi wote wa vyuo vikuu tumeliingilia kati swala hilo kwa kufanya
mazungumzo na uongozi wa bodi ya mikopo
HESLB pamoja na mh.Waziri wa
Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Ndalichako juu ya kubadili msimamo wa
muongozo huo kwakua utawaathiri wanafunzi wengi ambao ni watoto wa maskini.
Katika
majadiliano yetu yaliongozwa na hoja mbili zinazohusu wadahiliwa wapya na
wanaoendelea na masomo, tumekubalina yafuatayo:
1. Muongozo
mpya wa utoaji mikopo uliotolewa kwa mwaka huu wa masomo 206/2017 utawahusu
wadahiliwa wapya wanaoanza masomo.
2. Wanafunzi
wanaonufaika na mikopo wanaoendelea na masomo wao wataendelea na utaratibu kama
ulivyokuwa tangu awali walivyoingia makubaliano na utaratibu mpya
hautawaathiri.
Hata
hivyo zoezi la serikali la kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi mnufaika anayestahili
kupata mkopo anapata mkopo wake.
Aidha
kufuatia Tangazo la Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia lililotolewa tarehe
17/10/2016 linalohusu uhakiki wa wanafunzi wanaoendela na masomo ya
shahada zoezi litakalofanyika kwa wiki
mbili kuanzia tarehe 19/10/2016. TAHLISO
inaomba kila mwanafunzi anayesoma shahada kuangalia majina yaliyotolewa kwenye
tovuti ya TCU ili kuhakikisha jina lake lipo,na kwa yule ambaye hataona jina
lake awasiliane na uongozi wa TCU haraka iwezekanavyo ndani ya wiki hizo mbili
kuanzia tarehe tajwa hapo juu ili
kuepuka usumbufu utakaojitokeza.
STANSLAUS
PETER KADUGALIZE
MWENYEKITI
WA TAHLISO
Subscribe to:
Posts (Atom)