CR7 amepiga hat-trick yake ya 43 zikiwemo 31 za LA LIGA TU katika mechi ya PRIMERA DIVISION leo dhidi ya DEPORTIVO ALAVES
Saturday, October 29, 2016
UJAZAJI WA DODOSO ZA MKOPO KWA WANAOENDELEA NA MASOMO
BODI YA MIKOPO - UJAZAJI WA DODOSO NDANI YA SIKU 30 - WANUFAIKA WA MIKOPO ELIMU YA JUU (KWA WANAFUNZI WANAOENDELEA)
KWA WANAFUNZI WOTE WALIOPO VYUONI
Wanafunzi wanufaika wa mkopo elimu ya juu..."hasa wale wanaoendelea na masomo",kuanzia jumatatu ijayo,tarehe 31/10/2016 kila mnufaika anapaswa kuingia kwenye akaunti yake binafsi ya HESLB ili ajaze DODOSO lililoboreshwa zaidi kwa lengo la kuwa na taarifa sahihi zaidi zinazoweza kuwa VERIFIED na vyombo vya serikali kuhusu hali ya kifedha ya mnufaika.
Baada ya dodoso hilo kujazwa, litahakikiwa na ikibainika taarifa ulizotoa ni za uongo basi mnufaika ATAPOTEZA SIFA ya kupata mkopo wake.
Pia, kwa yoyote ambaye hatajaza DODOSO hilo pia naye ATAPOTEZA sifa ya kuwa mnufaika. Kwa hiyo ni zoezi la VERIFICATION ya taarifa za kifedha za mnufaika. Muda ukifika Dodoso hilo litajieleza.
Hivyo, from next Monday every beneficiary has to log into his/her account. Ni zoezi la muda wa mwezi mmoja tu na litaisha mwezi Novemba hivyo kila mtu afanye hima kujaza dodoso hilo jipya.
Pia unatakiwa kuendelea kuhakiki majina yenu (Kuna ya mwaka wa kwanza na wanaoendele). ili kujua kama upo chuo kihalali (kwa sifa na vigezo) au la. Zoezi hilo limeanza tayari. - hii ni kwa wanafunzi wote
SERIKALI YARUDISHA HISA ZAKE UDA
Serikali imefanikiwa kurejesha udhibiti wake kwenye Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) baada ya kurejeshewa asilimia 52 ya hisa zilizonunuliwa kinyume na utaratibu na Kampuni ya Simon Group Limited (SGL).
Kurejeshwa kwa hisa hizo kunatokana na ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwamba mauzo ya hisa hizo yaliyofanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa Uda hayakuwa na kibali cha Serikali.
Ripoti ya CAG ya mwaka 2014/15 ilibainisha licha ya utaratibu kukiukwa pia hakuna vilelezo vya fedha za manunuzi zaidi ya kuonyesha Sh320 milioni ziliingizwa kwenye akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Bodi, Idd Simba ambazo hata hivyo alidai ni malipo ya ushauri alioutoa kwa mwekezaji huo.
Kurejeshwa kwa hisa hizo, kutolewa taarifa ndani ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ambayo Jumanne ya wiki hii iliuweka kikaangoni uongozi wa Jiji la Dar es Salaam kuhusiana na sakata la Uda.
Pia, kamati iliwataka Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) George Simbachawene, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru wafike kwenye kamati wakiwa na majibu sahihi kuhusu sakata hilo.
Viongozi hao waliitikia wito huo jana, na baada ya kikao cha faragha Mwenyekiti wa LAAC , Vedasto Mwiru alisema Serikali imeitaarifu kamati yake kuwa imerejesha katika himaya yake fungu kuu la hisa ambazo hazikugawiwa.
Mwiru alisema Serikali imerejesha hisa asilimia 52 ambazo ziliuzwa na Bodi ya Wakurugenzi Wa Uda kinyume cha utaratibu.
“Maelezo yaliyotolewa na Serikali zile share (hisa) zote ambazo hazikugawiwa ziko salama chini ya mikono salama ya Serikali hazijauzwa,” alisema.
Mwiru ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CUF), alisema kutokana na maelezo hayo wabunge wametaka mikataba ya kurudisha hisa hizo kwa Serikali ipelekwe kwenye kamati hiyo.
Alisema kamati hiyo inaipa Serikali muda wa wiki mbili kuhakikisha kuwa wanawasilisha nyaraka hizo.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema wanasubiri majibu ya barua yao ya kuomba ushauri kuhusu uuzwaji wa hisa za jiji za asilimia 51 kutoka kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Alisema baada ya kupokea ushauri huo watapeleka katika Baraza la Madiwani ili kuona namna ya kwenda mbele pamoja na kuzifanyia kazi fedha walizouza hisa zao ambazo ziko katika Benki Kuu (BoT).
Mwanasheria Mkuu Masaju alisema anakwenda kuandika mambo yote yaliyosemwa ili iwasaidie kamati na Jiji la Dar es Salaam kukamilisha utaratibu huo kisheria.
Subscribe to:
Posts (Atom)