Saturday, December 3, 2016

AJIRA KWA WALIMU

Baada ya serikali kusitisha utoaji wa ajira mpya ili kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma nchi nzima.Imepanga kutoa ajira mpya kwa waalimu 35,000 katika mwaka wa fedha wa 2017/2018. Hayo yamesemwa Disemba 2, 2016 na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo katika kikao cha maelekezo ya utendaji kazi kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Jaffo amesema watakao ajiriwa ni wale waliohitimu kozi za ualimu mwaka jana na watakaohitimu mwaka huu.