Friday, November 4, 2016

UPASUAJI WA KWANZA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA

Kenya imekuwa nchi ya kwanza kufanya upasuaji wa kwanza wa kuungana kwa watoto kufanikiwa miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara kuweza kuwafanyia upasuaji watoto wawili waliozaliwa mwaka 2014 ambao walikuwa wameunga sehemu ya chini ya uti wa mgongo kwa muda wa miaka miwili. Watoto hao walikuwa na viungo vyote sawa isipokuwa sehemu ya kujisaidia haja kubwa ndio walikuwa wakichangia moja kutokana na tatizo ilo la kuungana.

MSAKO WA WADAIWA SUGU HESLB KUANZA KARIBUNI

Bodi ya Mikopo itatangaza majina ya wadaiwa sugu kuanzia mwaka 1994 ambao madeni yao yameiva.
Majina ya Wadaiwa sugu yatawekwa hadharani tarehe 13 Novemba, 2016.  Wasugu hao watapewa siku 30 kulipa madeni yao.  Baada ya muda huo, hatua za kisheria zitachukuliwa na wahusika watalipia gharama za kuwasaka.
Kwa mawasiliano zaidi piga 0763 459165 au 0767 513208

Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
03/11/2016