UKWELI KUHUSU NDEGE BUNDI
Uwezo wa Bundi kutambua Kifo cha Mtu
Bundi ni aina ya ndege ambao hula nyama; hufanya mawindo yao wakati wa usiku na kupumzika wakati wa mchana.
Pamekuwa na imani kwa wengi kwamba bundi anapoonekana nyumbani kwa mtu basi ni lazima kuna mtu atakufa katika nyumba hiyo.
Hivyo imewapelekea watu wengi sanaa kuwa na hofu kubwa juu ya kiumbe hiki cha Mungu na hivyo kukihusisha na nguvu za giza kwamba ni lazima ametumwa na mchawi kuja kuchukua roho ya mtu.
UKWELI UPO HIVI:
Bundi ana uwezo mkubwa sanaa wa kuvuta harufu ya mzoga kutoka mbali.Uwezo huu wa kunusa harufu unapita uwezo walionao binadamu.
Hivyo inapotokea katika nyumba fulani kuna mgonjwa mahututi ambaye seli zake za mwili wake zimeshaanza kufa lakini mapigo ya moyo bado yanafanya kazi ;Bundi huweza kunusa harufu ya seli hizo, harufu ambayo binadamu hawawezi kuhihisi, na hivyo huvutiwa kuisogelea kwa ajili ya kujipatia chakula ila hataweza kuingia ndani kwa kuhofia binadamu.Kwa kawaida binadamu hafi mara moja, bali hufa hatua kwa hatua. Zinaanza kwanza kufa seli za mwili,badae ogani mbalimbali za mwili.
Ogani za mwisho kufa huwa ni moyo ikifuatiwa na ubongo. Hivyo bundi anapoonekana katika nyumba yenye mgonjwa mahututi ni dalili kwamba mgonjwa huyo ameshaanza hatua za kufariki, na hivyo uwezekano wa mgonjwa huyo kufariki siku za karibuni ni mkubwa sanaa.
Inapotokea kwamba mgonjwa amekufa baada ya bundi kuonekana, tafsiri sahihi sio kwamba kifo hicho kimesababishwa na bundi bali ni kwamba dalili za kifo cha mgonjwa huyo zimetambuliwa na bundi.
Hivyo cha kufanya sio kumtafuta mchawi nani bali ni kuzidi kukabidhi mgonjwa huyo katika huruma ya Mungu kwa njia ya sala. Na hofu hii ya kuwa bundi anahusiana na nguvu za giza ipo zaidi Afrika lakini ulaya na mabara mengine hawana hofu hiyo maana wao humtazama Bundi kama ni kiumbe tu cha Mungu.
Zipo mbuga nyingi duniani ambazo hufuga bundi na watu wengi hupendelea kumtazama kwa sababu ya sifa yake kubwa ya kuweza kugeuza shingo yake kutoka mbele mpaka nyuma pasipo kuhitaji kugeuka kwa kiwiliwili chake.
Na mwisho kabisa nipende kusema kwamba hatupaswi kuwaogopa wala kuwachukia bundi ama kuongea vibaya juu yao kwa maana hao pia ni viumbe wa Mungu kama walivyo njiwa,kondoo , kuku n.k.Na kuongelea vibaya juu yao ni kuongelea vibaya juu ya kazi ya Mungu ya uumbaji wake.
Na Dr.Amani L.Mang'alila
Animal Behavior and Psychology
Dodoma-Tanzania