Friday, December 9, 2016

Maadhimisho ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania


Picha 16 za Maadhimisho ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara Yaliyofanyika Jijini Dar

Mabweni ya shule ya Secondary ya Ufundi ya Mtwara Yateketea Kwa Moto


Bweni la wasichana wa shule ya sekondari ya Mtwara ufundi iliyoko katika Manispaa ya Mtwara Mikindani limeteketea kwa moto leo majira ya saa moja asubuhi.

Akizungumza katika eneo la tukio kamanda polisi Mkoani hapa Thobias Sedoyeka amesema kwamba majira ya saa moja katika shule ya sekondari ufundi kulitokea moto ambao ulianza kuwaka katika mabweni ya wasichana ambapo mpaka sasa chanzo hakijajulikana na kuongeza kuwa hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu na makadirio ya hasara ya thamani ya jengo na mali zilikuwemo  bado haijajulikana.
 
Naye mwalimu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Nanyalika amesema kwamba alikuwepo eneo la tukio wakati bweni hilo la wasichana wa shule ya sekondari ya ufundi linaanza kuteketea ambapo kwa upande wake hajui chanzo cha moto huo hali ambayo imepelekea walimu ambao wanaishi ndani ya shule hiyo kuwa na hali ya sintofahamu kwa kuhofia usalama wao.
 
kwa upande wake mwalimu wa shule ya sekondari Sululu Sekondari iliyoko Mjini Masasi ambae yupo shuleni hapo kwa ajili ya kusahihisha mitihani ya kidato cha pili na alikuwa akitumia moja ya chumba cha bweni hilo amesema kwamba kipindi ambacho wapo katika maeneo yao ya kazi ndipo walipoona moshi unatokea kwenye bweni.
 
Naye mwalimu Masele Francis kutokea shule ya sekondari ya Namwombe iliyoko katika Halmashauri ya Masasi ameeleza kuwa kipindi ambacho anatoka bwenini aliona moshi mkubwa hali ambayo ilimpelekea kurudi ndani ili kuwapa wenzake taarifa.
 
Aidha  Afisa Habari wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi.Jamad Omary amewatoa hofu walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo na kuwaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu mbali na hayo amewataka wananchi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani kuwa na ushirikiano wa kutosha pindi kunapotokea tatizo kama hilo na si kuishia kutoa lawama.
 
Hata hivyo Kamanda amesema kwamba taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo ikiwemo chanzo cha moto huo itatolewa baada ya taratibu zote kukamilika.


Wednesday, December 7, 2016

Rais Magufuli Aongoza Kikao

Rais Magufuli Aongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu Dar es Salaam

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo tarehe 07 Desemba Ikulu jijini Dar es Salaam. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU

NEC yatangaza chaguzi ndogo

NEC yatangaza ratiba ya chaguzi ndogo za Ubunge na Madiwani

Na Eliphace Marwa – MAELEZO
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza ratiba ya uchukuaji wa fomu za kujaza nafasi zilizo wazi ya Mbunge na Madiwani katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Imesema kuwa inatarajia kuendesha Uchaguzi Mdogo katika Jimbo la Dimani , Mkoa wa Mjini Magharibi ,Tanzania Zanzibar kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Tume hiyo, hatua hiyo itanatokana na vifungu vya 37(1)(b) na 46(2) vya sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Vifungu vya 13(3) na 48(2) vya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura 292.

Aidha ,Tume hiyo pia itaendesha Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi za wazi za Udiwani katika kata 22 kwenye baadhi ya Halmashauri za Tanzania Bara zilizokuwa wazi kutokana na sababu mbalimbali.

Imezitaja Kata hizo Ng’hambi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Ihumwa ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Kiwanja cha Ndege ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Igombavanu na Ikweha za Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa pamoja na Ngarenanyuki iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha.

Kata nyingine ni Kijichi ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam, Kata ya Kinampundu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida, Isegehe ya Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga, Kasansa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi, Malya na Kahumulo Mkoani Mwanza, Maguu na Tanga Mkoani Ruvuma pamoja na Kata ya Kimwani Mkoani Kagera.

Imeongeza kuwa Kata nyingine ni pamoja na Nkome Mkoani Geita, Kata ya Lembeni Mkoani Kilimanjaro, Mkoma ya Mkoani Mara, Duru ya Mkoani Manyara, Mwamtani ya Mkoani Simiyu, Misugusugu ya Mkoani Pwani pamoja na Mateves ya Mkoani Arusha.

Tume hiyo imesema kuwa zoezi la kutoa fomu za uteuzi litaanza Desemba 10 hadi 22 na kufuatia kwa zoezi la uteuzi wa wagombea siku ya tarehe 22 mwezi Desemba na Desemba 23 hadi Januari 21 mwakani itakuwa ni kipindi cha kampeni ambapo Januari 22 mwakani itakuwa siku ya kupiga kura.

Simulizi ya Msamaha wa Mama – 06


global-insta
MWANDISHI/MTUNZI SEID BIN SULTAN
NILIONGEA kwa huruma na sauti ya chini kwani tayari nilishahisi kuna kitu nimemkosea mUme wangu na mimi nIlikuwa sipendi nimkosee kwa lolote.
Nilipomuuliza hivyo aliniangalia sana kwa jicho la husuda mpaka niliogopa, alionekana kuwa mtu aliyejawa hasira, aligeuka akanipa mgongo kisha akanambia, “Sihitaji kuzaa kwa sasa…”
Ni jibu ambalo lilinifanya jasho lianze kunitoka kabla hata ya kumuuliza kwa nini, nilihisi tumbo linauma, mwili wote uliishiwa nguvu, nilitoa macho na kumuuliza kwa sauti ya upole.
“Kwa nini hutaki kuzaa?”
“Sihitaji maswali, bali nimekwambia sitaki kuzaa, nielewe mwanamke!” alinijibu hivyo baada ya kumuuliza.
Alitoka akaingia chumbani, nilijaribu kumuita mme wangu lakini hakuitika, nilijua labda ananitania ilibidi nimfuate chumbani, nilimkuta amelala chali miguu chini akiwa hajavua viatu.
Ilikuwa kawaida yangu kila siku kumvua viatu kwa sababu tayari nilishakubali kuwa mjinga kwake ili kulinda ndoa yangu. Niliteremka chini nikiwa katika hali ya unyonge, nikamvua viatu vyake pamoja na soksi, nilisogea na kumuuliza tena, machozi yakiwa yananilengalenga.
“Mume wangu, uko serious kwa ulichoniambia au unanitania?”
“Sihitaji kuongea chochote, niache nipumzike,” alisema kwa mkato.
“Mume wangu hali yangu si nzuri niambie ukweli basi; please ongea chochote kile kingine kizuri, nionee huruma mwenzio. Nilisema kwa sauti iliyokuwa imejaa upole.
“Mwanamke nielewe, sihitaji kuzaa kwa sasa,” alisema.
Niliumia sana kusikia hivyo, kwa mara ya pili machozi yalianza kunitoka kama mtoto, aligeuka na kulalia tumbo nikasikia akisema maneno yaliyonifanya nitake kulia.
“Tena hiyo mimba nataka uitoe haraka iwezekanavyo!”
“Unasemaje Masoud!!?” nilimuuliza kwa mshangao.
“Si matangazo ya vifo!  Umepewa masikio ili kusikia,” alijibu kwa kunikejeli.
“Masoud unanijibu hivyo mimi leo!  Kwa kipi kibaya hasa nilichokufanyia?”
Kuanzia siku hiyo alianza kubadilika, nyumbani alikuwa akirudi muda  anaotaka, ilifika kipindi akawa analala chumba chingine nikimuuliza kwa nini anasema, “Toa mimba!”
“Toa mimba” ndiyo ukawa wimbo uliobakia nyumbani, hakukuwa na salama tena kisa mimba, nikafika sehemu nikachoka maneno yake. Nakumbuka alikuwa anajiandaa kwenda kazini, nikamwambia naomba niende kliniki kuandikisha.
Aligeuka na kuniangalia, akaniuliza nasemaje? Nikarudia tena nilichomwambia, aliniangalia bila kupepesa macho zaid ya sekunde nne kisha akasema.
“Nimesema, toa, hiyo, mimba!”
“Hivi Masoud kwa nini unakuwa hivi mume wangu ee?  Kuna familia inahitaji watoto, kuna wanawake hawajapewa kizazi wanalilia kila siku mtoto, leo mimi nimejaaliwa kupata mimba unasema nitoe kwa nini lakini?  Tena ni ya halali mume wangu hatujazini sisi au ulinioa kwa ajili ya starehe zako binafsi?”
“Yyees nilikuoa kwa ajili ya starehe,” alisema Masoud kwa hasira… na bora ningeoa mgumba kwa sababu sihitaji kuzaa, kwa nini ung’ang’anie wakati staki lakini.?  Sihitaji kuzaa mwanamke, kwani lazima? Usipoitoa hiyo mimba mtafute baba yake mimi sio.”
“Masoud naomba usinifanyie hivyo, kwa nini lakini unanifanyia hivyo mimi, kwani  kitu gani hasa kikubwa kinakufanya hivyo ee?”
Nilianguka chini nikamshika miguu.
Sikuamini kama Masoud anaweza kunipiga siku moja, lakini siku hiyo kudhihirisha kuwa hayuko tayari kuzaa na anaichukia mimba yangu, alinigeukia akanisukuma kitandani na kuanza kunipiga ngumi za tumbo huku akilalamika.
“Kwa nini hunielewi wewe mwanamke, au mpaka nikuue ndo uamini?  Sitaki, sitaki, sitaki, sitaki mpumbavu wewe, sasa kwa kuwa hutaki kutoa ngoja niitoe mimi, alaaaa unanletea upuuzi hapa!”
Kila aliposema  hivyo, alikuwa akinikandika ngumi za tumbo zilizopelekea kuzimia.  Jasho lilikuwa likimtoka, aliniacha bila kujali akaenda kazini, nilipozinduka nilishangaa kuona tumbo linaniuma sana, nilitoka nikaenda hospitalini, daktari alinipima akanipatia dawa na kunishauri nipumzike.
Nilirudi nyumbani nikiwa natokwa na machozi, kibaya zaidi nilikuwa sijui kwa nini Masoud alibadilika kiasi hicho.  Kiukweli niliumia sana, nilihisi dunia ni chungu ndani ya muda mfupi, nilitamani kufa kwa hali niliyokuwa nayo. Bado sikuacha kumjali mume wangu, niliamini ipo siku Mungu atanisaidia na kama mali ndiyo zimemfanya awe hivyo basi atamkumbusha kuwa anakosea, atajirekebisha.
Ulikuwa ni usiku wa tarehe mbili siku ambayo sitoisahau katika maisha yangu, alikuwa ameingia bafuni kuoga, simu yake iliita nikasogea karibu kuiangalia nikakutana na jina Yulaina kwenye skrini.
Nilishtuka kidogo baada ya kuangalia saa nikakuta ni saa tano usiku, nikajiuliza ni nani huyu anayempigia mume wangu usiku wote huu! Nilinyanyua simu nikapokea, nikaweka sikioni kisha nikakaa kimya kusikia ataongea nini.
Moyo wangu ulianza kuuma na kujuta kwa nini nimepokea niliposikia akisema,  “Hello Darling,  how are you?”  Sikuongea chochote nikijua huenda ataongea kitu zaid ya hicho, na kweli baada ya kuona nimekaa kimya akasema.
“Sweet, mbona kimya?  Au uko na hicho kijimwanamke chako?  Kama nlivyokuambia naomba usifanye nacho mapenzi, ikifika asubuhi kabla ya kuingia kazini njoo upate vitu vitamu huku ambavyo hakajawaki kukupatia, si unanijua shughuli yangu?  Habari nzuri ambayo nadhani ni kiunganishi kizuri cha mapenzi yetu ni kwamba nimeenda kupima leo nimeambiwa nina kabebi tumboni natamani uwepo ukashikeshike katumbo kangu!”
Sikuweza kuvumilia, miguu ilishika ganzi nikaishiwa nguvu, nilifanikiwa kuiweka simu kwenye meza nikaanguka chini.
Alipotoka bafuni aliniita huku akinimwagia maji ya baridi, nilishtuka nikalala kitandani, aliniuliza kulikoni nikamwambia hakuna ni mshituko tu, kabla sijamaliza kuongea simu iliingia tena, aliichukua na kutoka nayo sebuleni, ikabidi nami nisogee nisikie atachokiongea.
“Hello beibi!” alisema Masoud.
“Mbona simu yangu ulikata?”
“Acha jokes bhana, mi nilikuwa naoga beibi, nambie!”
“Sina la kukuambia zaidi ya kukuambia tena kesho asubuhi pita uje ukaage katoto kako tumboni nimeenda kupima nina pregnancy!”
“Weeeee!  Sema, hakya-Mungu!.
“Hakya-Mmungu sweet nina mimba yako!”
“Heheheeee!  We mtoto mbona unataka kunifanya nimkimbie huyu mwanamke?  Si kesho, nakuja sasa hivi kukaangalia kabebi kangu, sasa hivi nakuja, sawa mamaa?”
“Haya njoo sweet, nitakuwa na amani zaidi.”
“Niko kwa ajili yako mmmwwaaaa!”
Alikata simu na kuja haraka chumbani, mimi nilimuwahi nikakaa kitandani, alianza kuvaa nikamuuliza andkwenda wapi, akajibu, “Haikuhusu.”
Nilishindwa kuvumilia, nilitoka hadi mlangoni na kumwambia Masoud haendi kokote, alinangalia na kuniambia mara tatu akiomba nimpishe, akaanza kunipiga makofi ya masikio, akanisukuma nikaangukia chini naye akapita na kuondoka zake.
Nilianza kulia kama mtoto, siku hiyo sikujua nililala saa ngapi, aliporudi siku ya pili tayari nilishaandaa chai, nilimkaribisha vizuri kama mtu asiyejua chochote, nikamuuliza kwa kujiamini nikiwa katika hali ya kawaida.
“Mke mwenzangu hajambo?”
“Nini?”  alishangaa sana kumuuliza hivyo.
“Marudio Jumamosi, kama hujasikia limepita karibu unywe chai,” nilimjibu.
Ilibidi nimjibu vibaya siku hiyo kutokana na hasira nilizokuwa nazo kwa sababu nilishaona tayari ninakoelekea ni kubaya, nilijuta kwa nini Masoud alipata mali, kwa kuwa tayari nilishajua kuwa kuna mwanamke mwenzangu ambaye sikujua kama amemwoa au laa, ilibidi nipunguze wivu.  Kibaya zaidi nikajua hayuko tayari kuzaa na mimi ila yupo mwanamke mwengine ambaye yuko tayari kuzaa naye.
Nlipomjibu hivyo aliniuliza.
“Naona una hamu ya kupigwa,  siyo?”
“Nishazoea kupigwa kwa sababu umenigeuza ngoma, kila ukijisikia unapiga tu.”
Aliniangalia kwa jicho baya, aliachia msonyo na kuingia ndani.
“Utasonya sana mwaka huu, nishaujua ukweli wala hunibabaishi, japo naumia lakini nitafanyaje.”
Niliongea kwa kujipa moyo lakini maumivu bado yalikuwa yakinisumbua, machozi yalianza kunitoka upya, nilimimina chai nikajaribu kunywa lakini haikunyweka nikasukumia kikombe mbali kwa hasira.
Kila siku alizidi kunifanya matukio mapya mabaya.  Alizidi kunifanyia mapya, nilikuwa nikienda kupima hospitali kila kukicha, madaktari walinipa ushauri mzuri namshukuru Mungu, kwa kuwa ndiyo ilikuwa mimba yangu ya kwanza nilifatilia ushauri wao mwanzo-mwisho, nilienda kwa wataalam wa ushauri ili kurudisha amani ndani ya ndoa yangu lakini haikuwezekana.  Nilipoenda kwa wazee wake kumbe tayari alishawambia wote  kuwa anataka kuoa mke mwengine ambaye ndiyo mwema kwake na mjanja, walinishambulia kwa maneno tofauti mabaya, nikawa mtu wa kulia kila siku kila kukicha.
Ilikuwa ni siku nyingine tena mbayo sitoisahau katika maisha yangu, nilipokuwa jikoni,  napika jamaa aliniita nami nikaitika, nikaenda sebuleni na kukutana na sura ya mwanamke wa Kiarabu.
Nilimuangalia mwanamke huyo, huku mme wangu akiwa amekaa kwenye kiti anatingisha miguu, nilimsalimia mume wangu na kumkaribisha huyo dada. Kilichonishangaza baada ya kumwambia hivyo alinisonya ‘akanishusha na kunipandisha’, mume wangu alicheka sana,  moja kwa moja nikajua uenda huyo ndiye Yulaina.
“Najma!” aliniita Masoud nami nikaitika.
“Abee,” niliitikia kwa upole.
“Huyu anaitwa Yulaina, mtoto mzuri kuliko wote duniani , mtoto wa Kiarabu, mtoto mwenye hadhi ya kukaa kwenye nyumba nzuri kama hii. Yaani alivyoingia tu na nyumba imecheka kwa sababu ameendana nayo, kama unavyomuona akikaa kwenye sofa anajaa kama jini vile. Heheheee, vipi tumependeza ee!!!” alisema.
Sikuweza kuvumilia, hasira ziliniingia nikamwambia basi inatosha, nilitoka pale na kuingia ndani chumbani,  nikapakia nguo zangu kwenye begi machozi yakiwa yakinitoka, hapo tayari nilikuwa na mimba ya miezi mitano na nusu. Nilitoka ndani hadi sebuleni mwili wangu ukiwa hauna nguvu>  Nilijaribu kufuta machozi yaliyokuwa yanatoka lakini ilishindikana, nikiwa na begi nilimuangalia Masoud nikamwambia,
“Asante sana, nashukuru Masoud, Mungu akuongoze, inshallah atanilipia kwa yote niliyokufanyia kama mke, na hiki kiumbe kilichoko tumboni ipo siku moja utakifuata tu hali ya kuwa hakikutambui, na hicho kiungo kilichoko mwilini mwako kitakutafuna tu.”
Aliniangalia akiwa anacheka, kabla sijatoka nje aliniita na kuniambia.
“Cha kukusaidia tu ngoja nikuandikie talaka zako zote tatu na usahau kuhusu mimi kwa sababu hatuendani, jingine kama hutojali, najua pakuishi patakuwa tabu kidogo kwa sababu huyo mama yako ana kanyumba kana chumba kimoja tu, tena si kanyumba nimekuheshimu, ni  kijibanda,  nakuachia shamba la huko kijijini uishi humo na ni lako hilo nimekupa.
“Ninavyokupenda nakupa na mkataba wake huu hapa, nakupatia bure si langu mimi hilo silitambui ila tu nitakuja kuvuna kila kilichomo ili upande vya kwako, wasalimie uendako siwezi kuwa na mwanamke wa Kiswahili mimi, nahitaji mwanamke anayejua kutumia bhana.
“Mtoto mzuri huyu hapa kwanza kimahaba humshiki, akiwa kitandani anashugulika kweli, si wewe dakika mbili eti mume wangu nimechoka, mashine hii hapa toto kuanzia mwili hadi ladha ni sweet, si wewe unaniita sweet huku hujui kitu.”
“Nashkuru sana Masoud,” nilimjibu.
Hilo ndiyo jibu nililompa baada ya kuniambia aliyoniambia, nilitoka nje na kukutana na kundi la ndugu zake wote, waliniangalia na kuachia kicheko nikapishana nao wakiingia ndani, nilisikia kauli tofauti wakizisema, moja ambayo niliishika mpaka kesho.
“Yamekushinda, ondoka usiwabane wanaoweza kuyahimili.”
Nilitoka na maumivu makubwa  ambayo sitoyasahau hadi kufa kwangu, na hakuna siku nitakayoumia kama siku hiyo katika maisha yangu yote.
Machozi yalizidi kunitiririka wakati wote, nilipofika getini nilikutana na mlinzi wa geti,  tayari naye alikuwa analia kutokana na huruma aliyokuwa ananionea, kwani niliishi naye vizuri na kumchukulia kama ndugu yangu.  Alinikumbatia na kuomba nimpatie namba yangu ya simu, nilimpatia, naye akatoa kiasi cha shilingi laki moja akanipatia, nilishukuru sana.
“Sitoweza kupata bosi aliyekuwa na huruma kama wewe, nitakukumbuka daima, ila konga moyo wanaume ndo tulivyo hasa tukishapata pesa. Nilikuchukulia kama dada’angu wakati ni bosi wangu, nimeshuhudia mengi ukifanyiwa ndani lakini ulivumilia, muda wote nilikuwa nikikuonea huruma bosi unavyoteswa na mumeo, ila ya Waswahili hatimaye yametimia.
Kiukweli nami nahisi sitoweza kuendelea na kazi hapa, bora nikose kibarua kwa ajili yako madam, naomba unisubiri hapo nje niende nimwambie nimeacha kazi ili japo tuongozane nipajue utapoishi kwa sasa, tuendeleze udugu wetu kwa sababu umenisaidia mengi sana ambayo yalinifanya nikuone wewe ni miongoni mwa watu wachache ambao bado wapo katika dunia hii ya sasa.
TUKUTANE SEHEMU YA 07 

Saturday, December 3, 2016

AJIRA KWA WALIMU

Baada ya serikali kusitisha utoaji wa ajira mpya ili kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma nchi nzima.Imepanga kutoa ajira mpya kwa waalimu 35,000 katika mwaka wa fedha wa 2017/2018. Hayo yamesemwa Disemba 2, 2016 na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo katika kikao cha maelekezo ya utendaji kazi kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Jaffo amesema watakao ajiriwa ni wale waliohitimu kozi za ualimu mwaka jana na watakaohitimu mwaka huu.

Wednesday, November 30, 2016

UKIMWI sasa kudhibitiwa

UKIMWI sasa kudhibitiwa kwa njia ya simu

Tanzania imeingia rasmi kwenye mfumo maalum wa kimataifa wa kupata huduma za afya ya UKIMWI kwa njia ya simu bila malipo mfumo ambao umefadhiliwa na nchi ya Marekani.

Akizindua mfumo huo Kaimu Balozi wa Marekani nchini Bi. Virginia Blaser amesema mfumo huo utawafikia zaidi ya watu laki nane huku lengo kuu la mfumo huo likiwa ni kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kutoka asilimia 7.5 mpaka asilimia 5 hadi kufikia asilimia 0.0.

Amesema watu wote ambao wanadhaniwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi hadi kufikia mwaka 2020 wawe tayari wamepimwa kwa asilimia 90, asilimia 90 waanze kutumia dawa, na asilimia 90 kiwango chao cha maambukizi kiwe kimepungua.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya TAYOA nchini Bw . Peter Masika amesema katika ufadhili wa mfumo huo wao wakiwa ni wasimamizi wa mfumo watahakikisha unawafikia watanzania wote hasa wale wasiofikiwa na huduma muhimu za kiafya na kuwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutumia mfumo huo ili kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi.

Chadema: Hatutakubali tena kudhulumiwa 2020

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) ,Vincent Mashinji amesema hawatakubali tena kudhulumiwa kwa namna yoyote  katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Dk. Mashinji amesema hayo huku akimtolea mfano wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, na kuongeza kuwa kuna mambo hutokea bila kutarajia lakini watapambana kwa kila hali,

“Huu ni uchaguzi kuna mtu alitarajia haya yaliyofanywa na Jecha? hii inaonyesha kwenye nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki, wewe umefanya mara ya kwanza tukanyamaza,ukafanya tena mara ya pili kibabe,tukalalamika, badala ya kutuita tuongee, unasema nendeni mkaseme kokote kule”alisema Mashinji.

Aidha, akiongelea utawala wa Rais Magufuli ,Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utawala bora na matokeo yake yeye ndio amekuwa kila kitu, ameongeza kuwa wakati anaanza  mapambano na rushwa aliamini kwamba angeweza kuliondoa tatizo hilo lakini imekuwa tofauti.

Hata hivyo, Mashinji ameongeza kuwa katika mwaka mmoja wa Rais Magufuli, amesema ameshindwa kusimamia utawala bora baada ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja na shughuli zote za kisiasa nchini kwa kile alichosema kuwa muda wa siasa umekwisha.

Sunday, November 27, 2016

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUSOMA "DEGREE" BILA KUPITA "FORM SIX".

Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katika mwaka ujao wa masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.

Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu.

Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi daraja la kati (Technicians). Lakini wale wanaokosa "credit" za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mwisho wao utakuwa diploma.

Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa.

"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako.


Saturday, November 26, 2016

SIMULIZI

“Kilitokea nini?
Ni swali nililouliza baada ya kuona amenifumba na mimi nilitaka kwenda nae sawa.
“Swali zuri, mwaka 1992 baba yako akiwa anatoka chuo baada ya kumaliza kufanya mitihani, aligongwa na gari lililokuwa linaenda mbio, na dereva kutokomea kusiko julikana, vijana walioliona tukio hilo walijaribu kulifatilia gari lililosababisha ajali na kukimbia bila kufanikiwa, haraka walimpeleka hospital ya mnazi mmoja darajani. Najma alipopata taarifa alizimia, alipozinduka aliomba aende hospital haraka akamuone mumewe kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwake.
Alipimwa ndani ya siku mbili, ndugu wa Masoud pamoja na Najma waliitwa ofisini kuelezwa kinachoendelea, ndipo waliambiwa anaitaji kuongezewa damu na figo ili kurudisha uhai wake kwani figo moja limekufa na lililobakia halina nguvu za kujitemegea.
Mjukuu wangu! ndugu zake wote waligoma kutoa damu kwa Masoud wakidai wana damu ndogo hata figo pia kumtolea walishindwa, mwanangu akasema bora nife mimi kuliko mume wangu, akaomba apimwe damu kama magroup yanaendana atatoa, na kama figo zake zote zinafanya kazi basi atatoa moja, alisema hivyo huku akiwa anabubujikwa na machozi na ishallah machozi aliyoyamwaga siku hiyo mungu atayalipa tu.
Docta alimuomba aingie kwenye chumba cha maabara, alipimwa damu na kukutwa ana group A kama Masoud na figo zake zote zilikuwa na uwezo wa kufanya kazi vyema, hivyo upasuaji ulianza mara moja wa kutoa figo na damu.
Walifanya upasuaji vizuri, baada ya siku kama tano hivi, Masoud akawa mzima, alimshukuru sana mke wake, walifurahi sana na maisha yakasonga mbele.
Baada ya miezi mitatu, matokeo ya vyuo yalitoka, masoud alipata  maks nzuri, akachaguliwa kuwa miongoni mwa wanafunzi bora wa chuo cha suza, matajiri wenye makampuni makubwa walimuita kwa ajili ya kuongea nae ili awafanyie kazi zao za kiofice, Mungu akamuwekea wepesi na kufanikiwa kujiunga na kampuni moja kubwa tu iko huko mjini.
Ilikuwa ni kama sherehe kwa najma, Hakuamini kama mme wake atapata utajiri wa mali ndani ya miaka michache kiasi hicho, aliinua mikono yake juu mwanangu na kumuombea mmewe kwa mungu ili mali zake ziwe na baraka.
Masoud baada ya kupata kazi kutoka kwenye makampuni yaliyokuwa yanaongozwa na wazungu, alikabidhiwa nyumba na gari la kutembelea, Walitakiwa wahamie mjini yeye na mke wake. ndugu wote waliitana wakaandaa kashuguli kadogo ka kumuombea dua. Alimchukua mkewe pamoja na ndugu zake wengine wakaenda mjini kupaona.
Najma hakuamini kama ipo siku moja angeishi kwenye nyumba ya kifahari haraka hivyo, siku ya kwanza alipofika alizimia zaid ya mara moja kwa sababu ya mshangao, wapo baadhi walimcheka kwa ushamba lakini haikuwa ushamba bali mazingira tu yalimchanganya, tokea kuzaliwa kwake alikuwa hajawai kukanyaga kwenye nyumba yenye mandhari nzuri..
Masiku, wiki, miezi ilikatika baada ya kuamia mjini, shida zote ziliwakimbia na utajiri kupisha hodi, unene ulianza kuiandama mili yao kutokana na kurizika na vyakula wanavyokula, namna walivyokuwa wametakata kwa pesa hukuweza kuwajua kirahisi kama ulipotezana nao miezi mitano au zaid.
Nakumbuka siku moja mwanangu alikuja kunitembea akiwa na gari dogo la kutembelea, tuliongea mengi akanipatia pesa za matumizi, ila katika maongezi yetu nkamwambia “mwanangu, mali hizo ni za mwanaume, siku yoyote anaweza kukuacha na wanaume wa siku hizi wasivyokuwa na haya,  anaweza asikupe chochote japo mali mmechuma wote, hivyo basi kuna kijishamba kinauzwa hapo jirani laki tatu na nusu, inabidi ukinunue kisha uweke watu wajenge japo kijibanda, maisha yanaweza kukushinda huko utakuja uendelee na kwako.
Mwanangu hakuwa mbishi, alinisikiliza ila akanambia sasa hivi hizo pesa hana akipata tu atakuja kulinunua, sasa sijui alisahau! au vipi maana sikumuona tena.
Maisha yao yalisonga mbele, shamba kubwa la masoud lililokuwa huku kijijini, kwa kuwa walikuwa hawaishi tena, nyumba iliyokuwa imejengwa ndani ya shamba iliendelea kuwepo, waliitwa watu wakalima mpunga, na mazao mengine ambayo walihisi badae yatawaingizia faida.
Mjukuu wangu mimi niishie hapo!!, mengine itabidi ukamuulize mama yako nahisi atakuambia, mbane usimpe nafasi japo yanamuuma lakini atakuambia tu kwa kuwa ushaupata mwanzo wake, akikusimlia yeye ni vizuri zaid kwani kuna vya siri nsivyovijua na wewe kwa kuwa unaonekana kuwa tayari una akili anaweza kukuambia, cha mwisho nnachokumbuka mimi, ilikuwa ni usiku wa tareeeeeeeee!  12 mwezi wa 5 mwaka 1993 ambapo tayari alikuwa na mimba yako, alikuja hapa akiwa analia na kijibegi flan hivi kidogo, kumuuliza kulikoni akasema “mama wee acha tu, sikuamini kama masoud anaweza kunifanyia hivi mimi? nliyoyashuhudia kwake yanatosha, na alivyonitesa mimi nkavumilia vyote na mwisho kudai talaka yangu mungu atanilipia tu, kwani nimemvumilia vya kutosha, kiukweli mamaangu bado siamini kama kupata mali tu angebadilika kiasi hiki.
sikuitaji kumuuliza zaid kwa sababu wanaume mi nawajua hasa wakishapata mali, sikumshauri akadai haki yake wala nini, kwa sababu asingeweza kutokana na upole alionao mamaako, nlichomuambia akae chini amuombe mungu wake atamsaidia, wasipolipana hapa duniani basi watalipana kwa mungu.
Ila kwa alichomfanyia kama amefanyiwa kweli mambo aliyoniadisia basi naamini ipo siku moja tu mungu ameipanga kwa kuwa malipo hapa hapa duniani!!, hatta siangaiki najua ipo siku na sisi tutacheka tu kumuona masoud akidhalilika, na kiungo cha mwanangu kilichoko mwilini mwake Nshallah kitamtafuna taratibu!. Alisema bibi.
“Bibi naomba unambie tu kila kitu nadhani mama hatoweza kunambia chochote mimi!
nliongea huku machozi yakinilenga, nlijikuta nkijuta baada ya muda mrefu kumuhisi mama vibaya kumbe alitendewa unyama kwa mujibu wa maneno ya bibi, bibi nae japo macho yalikuwa yakizee lakini yalianza kuiva alipokumbuka mambo yaliyomkuta mwanae, alinigomea kabisa kunambia chochote kilichoendelea, tayari nlishakuwa na mzuka wa kujua kila kitu kilichomtokea mama, sikupoteza muda nlimuaga bibi na kumuambia ntakuja kukusalimia kesho, nlitoka mbio mpaka ndani nkachukua baiskel yangu na kuanza kurudi nyumbani haraka, njia nzima moyoni mwangu kulikuwa na maneno ya” Lazima leo mama anambie ukweli wote sikubali, kumbe baba yangu ndo mshenzi wa tabia hayawani mkubwa!!!.
kama pedeli zingekuwa zinaongea nadhani siku hiyo zingeongea kuwa zinaumia kwa jinsi nlivyo kuwa nazikandamiza. Hazikupita dk kumi tayari nlikuwa nyumbani, nlishuka kwenye baiskel nkaiegesha kwenye mti wa korosho uliokuwa mbele ya nyumba yetu, nliingia ndani kwa kasi nkiita mama, mama tayari alikuwa shambani ikabidi nimfate huko huko.
nlipoingia shambani, nlimkuta anapariria, nkamuita. aligeuka na kunangalia huku akiniitikia.
” Shkamoo
“maraaba mwanangu umerudi baba.
“Ndio nimerudi, mama kuna kitu nataka tuongee ila ndani.
“um we mtoto mbona unavisa hapa haiwezekani kwani?.
“inawezekana ila naomba twende ndani.
“hhmm sawa.
aliniskiliza akanambia nichukue baadhi ya vitu. tulipoingia ndani alikaa kitandani kisha mimi nkavuta kisturi ili kumkalia kitako.
“Mama!, Naomba unisamehe mamaangu kwanza nimekukosea sana, siku zote nlikuwa nahisi uenda ulimtendea ubaya baba ndo maana hutaki kunambia chochote kuhusu yeye, ila bibi kaniambia kila kitu kilichokukuta na kunambia mengine utanambia wewe, nakuomba mamaangu unambie kila kitu kwani kufanya hivyo mimi ntapata msukumo flan wa kunifanya niwe na hasira za kusoma kwa bidii katika masomo yangu ili siku moja niwe na maisha bora, tafadhali mama.
Nlisema. Sikuweza kumuangalia machoni mama.
macho yake yalishabadilika nlipomtamkia maneno hayo, uso wake ulishakaa kihuruma, nlikumbuka maneno ya wahenga ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni, ukimwangalia unaweza kujikuta unashindwa kumuua na kukuua wewe.
“Mwanangu, bibi yako kakuambia kitu gani.?
aliniuliza kwa mshangao, nami nkamjibu.
“amenambia baba alivyokuoa mwaka 1990, mliishi kwa raha, matatizo yalianza alipopata mali, naskia alikutesa sana ndo maana ukarud nyumbani, hakuitaji kunambia vyote kwa sababu hayo mengine kasema hayajui vizuri, naitaji kujua ukweli wote mamaa! please nambie kila kitu mama angu niwe na amani, hata nkiwa natembea niwe najua ukweli wote nnao.
Mama hakuwa na jinsi, baada ya kusikia bibi ashanambia nusu, aliona haina maana tena akaamua kunisimlia kila kitu kilivyokuwa.
” Ni kweli mwanangu, baba yako anaitwa Masoud, ila namchukia kwa yale aliyonifanyia, na sikufundishi hata siku moja umchukie babaako kama utamwona, kwani waswahili wanasema mpende aliemtendea ubaya mtu muhimu katika maisha yako.
Sikuitaji kukuambia chochote kwa sababu ni story inayoniumiza ndani ya moyo wangu kila nkiikumbuka, na najaribu kuisahau moyoni lakini huwa nashindwa.
Babaako alikuwa ni mtu mzuri sana, alikuja kubadilika ghafla baada ya mimba yangu kuanza kukua, na sitomsameehe mpaka kiama kinasimama kwa alichonifanyia….
Mama alianza kulia, huruma iliniingia lakini nlionesha ukakamavu ili niujue ukweli wote hata nsiotakiwa kuujua nliitaji kuujua.
“nadhani bibi yako amekuambia mpaka tulivyohamia mjini. Alisema.
“Ndio mama
“Ok!! ni kweli tulihamia mjini mara tu baba yako alipoajiriwa kwenye kampuni kubwa na kupatiwa nyumba kubwa ya kuishi, nlifurahi sana nkijua ndo mwisho wa matatizo yangu, nliinua mikono juu na kumshukuru Mungu kwa kuniondolea tabu zilizokuwa zimenizunguka. bila kujua mabaya zaid yanakuja mbele yangu. hapo ndipo nlijua kweli ng’ombe wa maskini hazai na watu kama sisi tumezaliwa kwa ajili ya mikosi.
Tulikaa miezi sita kwa furaha huko mjini, hali yangu ilianza kubadilika kila leo bila kujua tatizo ni nini, kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo baba yako kwangu alinipeleka hospital haraka kupima vipimo vyote ndipo nkakutwa nna mimba ya mwezi mmoja.
Mme wangu alionekana mwenye furaha, tulikumbatiana mbele ya docta alietupatia majibu hayo, lakini nilishangaa kipindi tunarud nyumbani kwenye gari hakuniongelesha chochote na kila nlipomuongelesha hakujibu.
tulipofika nyumbani ilibidi nimuuliza.
“Tatizo nini mme wangu?
Nliongea kwa huruma na sauti ya chini kwani tayari nlishahisi kuna kitu nimemkosea mme wangu na mimi nlikuwa sipendi nimkosee kwa lolote.
Nlipomuuliza hivyo aliniangalia sana kwa jicho la husda mpaka nliogopa, alionekana kuwa mtu alojawa na hasira, aligeuka akanipa mgongo kisha akanambia ” SIITAJI KUZAA KWA SASA HIVI.”
TUKUTANE SEHEMU YA SITA……

Viongozi Atcl Wapanguliwa

Bodi  ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege nchini (ATCL) imewaondoa katika nyadhifa zao wakurugenzi wote waliopo katika menejimenti na baadhi ya mameneja, baada ya kubainika kuwa na kasoro za kiutendaji na kielimu.

Uamuzi huo, ambao hautamhusisha  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Ladislaus Matindi, ulitolewa katika kikao kilichofanyika Novemba 18, lengo likiwa ni kuboresha muundo wa ATCL, ili kukidhi matakwa ya muda mfupi wakati muundo wa kudumu ukiandaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya shirika hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Mhandisi Emmanuel Korosso, alisema katika kikao hicho bodi iliamua kuwaengua wakurugenzi watano waliokuwa katika idara mbalimbali, ikiwamo ya biashara, ambayo ilikuwa na kaimu.

Mhandisi Korroso alitaja idara nyingine ambazo wakurugenzi wameondolewa  kuwa ni fedha, usalama, ufundi na uendeshaji, ambayo mkurugenzi wake alikuwa anaelekea kustaafu.

“Kwakuwa wakurugenzi wengi walikuwa wanakaimu  nafasi hizo, tumeamua wakurugenzi wanaokaimu warudishwe katika nafasi zao  za chini, ambazo si menejimenti au wahamishiwe katika vituo vya mikoani,” alisema Mhadishi Korosso.

Alisema bodi pia imeagiza  kuondolewa kabisa katika shirika hilo wakurugenzi na mameneja waliothibitishwa ili waweze kupangiwa majukumu mengine yatakayoendana na sifa walizonazo.

Alisema kikao hicho pia kimemuagiza Mtendaji Mkuu kutangaza mara moja nafasi za wakurugenzi na mameneja zilizo wazi kwa kufuata muundo uliopitishwa.

Mbali na hilo, Mhandisi Korosso alisema kwa sasa shirika hilo limeweza kuongeza nidhamu katika mapato na matumizi, jambo ambalo limechangia kuanza kulipa baadhi ya madeni wakati Serikali ikisubiri uhakiki umalizike ili iweze kuyachukua.

“Tumeweza kudhibiti mapato na matumizi vizuri, kumekuwa na ongezeko la mapato ya uzito wa ziada wa mizigo kutokana na usimamizi mzuri, ukusanyaji wa mapato kutoka vituoni na mawakala umeboreshwa sana kutokana na ufuatiliaji wa karibu wa mauzo,” alisema Mhandisi Korosso.

Aliongeza kuwa, bodi pia imetoa ruhusa kwa wafanyakazi na familia zao kupewa tiketi bure mara moja kwa mwaka kama stahiki ya likizo na tiketi yenye punguzo mara moja kwa mwaka.

Kampuni ya ATCL, ambayo awali ilikuwa haina ndege hata moja, ilianza kufanya  kazi za safari za ndege Oktoba 14, mwaka huu, baada ya Serikali kununua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q400.

Monday, November 21, 2016

TCU Public Notice

TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES (TCU)

Public Notice

APPLICANTS WITH EQUIVALENT QUALIFICATIONS
TCU hereby informs applicants with equivalent qualifications whose names appear in the list that they are required to contact TCU not later than Tuesday, 22nd November 2016.

To view the list please click here...

They can contact the Tanzania Commission for Universities through the following numbers;

Landline: +255 (0) 22 2772657

Hotlines: +255 (0) 683 921 928

+255 (0) 675 077 673

Issued by;
Executive Secretary,
Tanzania Commission for Universities.

ORODHA YA MARAIS NCHINI MAREKANI

Obama Speaks

Obama says he may comment as citizen on Trump's presidency

  • 2 hours ago
  •  
  • From the sectionUS & Canada
  •  
  • comments

President Barack Obama and President-elect Donald Trump shake hands following their meeting in the Oval Office of the White House in Washington, Thursday, Nov. 10, 2016.Image copyrightAP
Image captionMr Obama and Mr Trump met at the White House two days after the election


By convention, former presidents tend to leave the political fray and avoid commenting on their successors.
US President Barack Obama has said he may speak out after leaving office if he feels his successor Donald Trump is threatening core American values.
Mr Obama said he would give Mr Trump time to outline his vision but added that, as a private citizen, he might speak out on certain issues.
Mr Trump spent the weekend interviewing candidates for top jobs in his cabinet.
"I want to be respectful of the office and give the president-elect an opportunity to put forward his platform and his arguments without somebody popping off," Mr Obama said at a forum in Lima, Peru.
But, he added, if an issue "goes to core questions about our values and our ideals, and if I think that it's necessary or helpful for me to defend those ideals, then I'll examine it when it comes".
The president described himself as an "American citizen who cares deeply about our country".